Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Kuandika maudhui bora ya kampeni

Wito wa kuchukua hatua unaopata matokeo bora


Hapa ndipo utakapowashawishi watu kuitia kampeni yako saini. Itumie fursa hii kulichambua tatizo, kuitambua suluhu na ni nani anayeweza kuitekeleza, na ueleze jinsi kuchukua hatua unayoipendekeza kunavyochangia katika kufanikisha suluhu hiyo. Ni jambo la busara kugusia maelezo yakini na marejeleo kutoka kwa vyanzo vinavyotambulika ili kuimarisha hoja yako. Watu wengi wasiolielewa suala lako lakini wanaotaka kusaidia hawatasoma maelezo marefu, kwa hivyo hakikisha unatoa muktadha kwa ufupi iwezekanavyo.

VIPENGEE MUHIMU

  • Suala kuu: Anza kwa kuangazia suala lako na mabadiliko yanayohitajika moja kwa moja, bila kupoteza wasaa. Huenda ikafaa kulieleza suala lenyewe kama la dharura na ambalo hatuna budi kulishughulikia.
  • Jukumu letu katika mabadiliko: hapa utaweka wazi jinsi kampeni yako itachangia katika kuleta suluhu uliyoibainisha -- mfikirie unayemlenga na jinsi shinikizo la umma linavyoweza kuchagia katika uamuzi wake.
  • Mwito: Hakikisha umemwalika msomaji kuchukua hatua unayoipendekeza. Pia ni muhimu kutoa maelezo yoyote mahususi ya ziada kuhusu mwito wako hapa.
  • Maelezo ya Ziada: Je, kuna chochote watakaounga mkono wanapaswa kujua? Labda kuna historia fulani amabayo unahitaji kuelezea au pingamizi ambalo unaweza kulijadili ili kutuliza hatihati zozote zilizo akilini mwa hadhira yako.

VIDOKEZO

  • Usiandike utangulizi mrefu badala yake liangazie suala unalolifanyia kampeni moja kwa moja (tunajua ni gumu! Shauku ya kunena mengi huwa kuu).
  • Angazia wakati na elezea -- mbona sasa? Dharura ya nini?
  • Tunasema ikiwa una shaka, itie kwenye taka -- ikiwa huna uhakika kuwa jambo fulani ni muhimu kujumuisha kwenye kampeni, kuna uwezekano mkuu zaidi kuwa si muhimu.
  • Izingatie hadhira yako -- unahitaji kuwahamasisha watu kutia saini, huku ukikumbuka kuwa unayemlenga huenda akautembelea ukurasa (hasa ikiwa shinikizo la umma limezidi).