×
KATIKA SEHEMU HII:
Msaada
Kuchagua picha
Wacha picha zikusaidie kunena
Picha inayofaa inaweza kusema yote pindi tu inapotupiwa jicho. Picha za kampeni zinaweza kuifanya kampeni yako kuwa ya kusisimua, kuvutia umakini wa watu, na kuwapa motisha ya kuchukua hatua. Hivi hapa vipengee mahususi vya picha za kampeni, zikiwa zimechaguliwa kutoka kwa mamia ya mifano na majaribio:1. REJELEA UBINADAMU WETU -- MWANGAZIE MTU FULANI
Maelezo ya taabu kuu ya kiuchumi barani Ulaya yanaweza kukosa kueleweka kwa urahisi, na umati wa waandamanaji unaweza kuwa ndiyo habari kuu badala ya kile wanachokifanyia maandamano. Kwa kumtia msichana kwenye darubini, picha hii inaleta akilini jinsi maamuzi ya kiuchumi yatakavyoathiri maisha yake ya baadaye pamoja na ndoto zake.
2. IAKISI KAMPENI
Kiini cha kampeni hii ni wanavyoumia watoto kupitia unyanyasaji usio na maana na wa kizamani wa mabomu ya nguzo -- na hilo linaonekana bayana katika picha yenyewe.
3. ONYESHA UPEO WA TATIZO
Salalaa! Miti hiyo inaonekana mikubwa kwelikweli na kuna mingi sana iliyokatwa. Picha hii inadhihirisha kiwango cha uharibifu wa mazingira unaofanyika nchini Brazili na kulifanya jambo linalotukia mbali -- kuangamizwa kwa msitu wa Amazoni -- kuwa kitu halisi (na ambacho ungependa kukomesha!).
4. MJUMUISHE MLENGWA WAKO
Kuiweka taswira ya mlengwa wako kama picha ya kampeni ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa analihisi joto la shinikizo kibinafsi -- hamna anayependa kukosolewa hadharani.
5. IFANYE YA KUPENDEZA MACHO
Rangi na mwanga katika picha hii zinavutia vilivyo -- halaiki ya watu walio na rangi nyekundu, ya chungwa, na manjano inazua hisi ya staha inayowasilisha nguvu na uchangamfu.
6. ONYESHA UKINZANI
Unapoitazama picha hii tu, unahisi kuwa hali hii haifai -- polisi waliovalia magwanda ya kutuliza ghasia wakiwasukuma wanawake, watoto na hata mkembe aliye uchi. Ulinganisho wa makundi hayo mawili unastaajabisha na unaonyesha dhuluma iliyopo ikiwa ni pamoja na tofauti kali kati ya wanaoandamana na jinsi serikali inavyoyajibu maandamano hayo.
7. KUTUMIA UTAMADUNI WA KISASA KUJITANGAZA
Chukua ishara au jambo fulani ambalo kila mtu analitambua na ulibadili ili liakisi ujumbe wa kampeni yako.
8. PICHA ZA KUOGOFYA SIO BORA VILE
Picha za kutisha na kuogofya au kuatua moyo, ingawa huzua hisia kali, zinaweza kutibua makini ya watu kutoka kwenye kampeni au kuwafanya watake kuuondokea ukurasa upesi. Picha hii maridadi ya tembo wakubwa iliisaidia kampeni ya kupinga ujangili zaidi ya picha ya ndovu anayefuja damu baada ya kuuawa.
Anzisha kampeni yako
Jukwaa jipya la Kampeni za Jumuiya ya Avaaz linasaidia maelfu ya watu kuanzisha na kushinda kampeni, katika ngazi za kikata, kitaifa na kimataifa!