Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Kutuhusu

Kuhusu Kampeni za Jumuiya ya Avaaz

Kampeni za Jumuiya ya Avaaz humwezesha kila mtu kutumia zana za mtandaoni ili kuchangia katika kuunda ulimwengu jinsi tunavyotamani ungekuwa.

Kampeni za Jumuiya ni jukwaa jipya la wavuti linalowapa watu duniani kote uwezo wa kuanzisha na kushinda kampeni katika ngazi za kikata, kitaifa na kimataifa.

Kampeni za Jumuiya ni sehemu ya Avaaz inayochangiwa na umati, na ni harakati kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani inayoleta siasa na sera zinazowazingatia raia katika maamuzi kila mahali. Kila juma, mamilioni ya watu wa asili mbalimbali na katika kila nchi duniani huchukua hatua kuhusu masuala muhimu, kuanzia ufisadi na umaskini hadi migogoro na mabadiliko ya tabianchi, kupitia Avaaz.

Muundo wa Avaaz wa uhamasishaji wa mtandaoni huwezesha maelfu ya juhudi za mtu binafsi, hata ziwe kidogo namna gani, kuunganishwa kwa haraka na za wengineo na kuwa nguzo ya nguvu ya pamoja. Kufuatia kuzinduliwa kwa Kampeni za Jumuiya, sote tunaweza kutumia zana hizi za mtandaoni ili kuendesha kampeni zetu wenyewe katika ngazi za kikata, kitaifa au kimataifa na zote kwa pamoja zitajumuika kuleta mabadiliko chanya duniani.

Avaaz — ikimaanisha “sauti” katika lugha kadhaa za Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia— ilizinduliwa mwaka wa 2007 kwa dhamira rahisi ya kidemokrasia: kuwaleta raia wa mataifa yote pamoja ili kuziba pengo kati ya ulimwengu tulio nao sasa na ulimwengu ambao watu wengi kila mahali wanautaka. Jumuiya ya Avaaz hufanya kampeni katika lugha 15, zinazohudumiwa na timu kuu katika mabara 6 na maelfu ya watu waliojitolea. Pamoja tunachukua hatua -- kutia kampeni saini, kufadhili kampeni za vyombo vya habari na hatua za moja kwa moja, kutuma baruapepe, kuzipigia simu na kuzishawishi serikali, na kuandaa maandamano na matukio halisi -- ili kuhakikisha kuwa maoni na maadili ya raia duniani yanaarifu maamuzi yanayotuathiri sisi sote.

Bofya hapa ili kufahamu zaidi kuhusu Avaaz